KING MAJUTO KUTOKA TANGA!
MSANII
mkongwe wa vichekesho Nchini Amri Athumani 'King Majuto'amesema kuwa
tangu ameanza kuigiza hajawahi kufikiria kuacha na wala hana mpango huo
ingawa umri wake ni mkubwa.Msanii huyo ambae pamoja na umri wake mkubwa
ana uwezo wa kuigiza nafasi zote ukitaka awe kijana nakua na ukitaka awe
mzee anakua. Alisema anawashangaa wanaofikiria kwamba ataacha leo au kesho kuigiza wamesahau kuwa hiyo ni kazi yake."Nawashangaa wanadhani nitaacha kuigiza leo au kesho eti umri wangu mkubwa mbona kwenye mashindano mbali mbali nawafunika"alisema Majuto.
Alifafanua kuwa pamoja na kuwafunika kwenye mashindano mbali mbali amekuwa halipwi fedha anazoahidiwa akishinda hivyo hataki tena kuitwa kwenye hayo mashindano uchwara.
"Nilishinda kwenyevshindano lililoandaliwa na Global Publishers lakini mpaka leo sijapewa zawadi yangu, wanaandaa mashindano bila kujiandaa matokeo yake kila nikishinda hawanipi changu hivyo sitaki tena na wakiniita siendi na ninawakumbusha mimi hii ndio kazi yangu kama alivyo Polisi .daktari ,mwalimu sasa kwani nini wanaidharau"alihoji Majuto.
Majuto alisema pamoja na misukosuko yote hiyo kupitia sanaa ya vichekesho amefanikiwa kujenga nyumba ya kuishi na anamiliki magari mawili.
No comments:
Post a Comment